Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Tangazo la Ajira

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Tangazo la Ajira

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia kibali cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/128/01/19 cha tarehe 10 Mei, 2018, inatangaza nafasi za kazi 1,500 za kada mbalimbali za afya kujaza nafasi za Wizara ya Afya, Wizara nyingine, Hospitali za
Rufaa za Mikoa na Taasisi za Umma kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Nafasi za kazi zinazotangazwa ni kama zifuatavyo:-

1. Assistant Technologist
2. Assistant Medical Officer II
3. Assistant Nursing Officer II
4. Assistant Technician
5. Biomedical Engineer Technician II
6. Biomedical Engineer II
7. Chemist II
8. Clinical Officer II
9. Dental Specialist II
10.Dental Surgeon II
11.Dental Therapist II
12.Environmental Health Assistant II
13.Environmental Health Officer II
14.Health Laboratory Scientist II
15.Health Recorder II
16.Health Secretary II
17.Launderers II
18.Medical Attendant
19.Medical Doctor II
20.Medical Specialist
21.Nurse II
22.Nursing Officer II
23.Occupational Therapist II
24.Opthalmic Optician II
25.Pharmacist II
26.Physiotherapist Assistant II
27.Physiotherapist II
28.Technologist II

Sifa za Waombaji

1. Awe Raia wa Tanzania
2. Awe na Umri usiozidi umri wa miaka 45
3. Asiwe mwajiriwa wa Serikali au mwajiriwa wa hospitali za mashirika ya dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali, endapo itabainika kuwa alishaajiriwa Serikalini na kupata cheki namba, mwombaji atatakiwa  kuzingatia utaratibu wa uhamisho au kurejea katika utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi ilivyobainishwa kwenye Waraka Na. CCB.228/271/01 wa tarehe 7 Agosti,2012.
4. Mwombaji awe na sifa kwa mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba 1 wa mwaka 2009 kuhusu kada zilizo chini ya Wizara ya Afya.

Maombi yote yaambatanishwe na:-

1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa
2. Nakala ya cheti cha kidato cha nne au cha sita kulingana na kada ya mwombaji
3. Nakala ya cheti cha taaluma
4. Nakala ya cheti cha usajili wa taaluma husika
5. Leseni ya kufanya kazi ya taaluma husika
6. Maelezo binafsi ya mwombaji (CV)
7. Picha ndogo (passport size) mbili za hivi karibuni

NB:
• Nakala za vyeti vyote vithibitishwe na Mahakama au Wakili
• Kwa waombaji watakaotuma maombi yao TAMISEMI hawapaswi kuomba nafasi hizi

Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta katika anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu (Afya),
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Chuo Kikuu cha Dodoma,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii,
Jengo Na. 11,
S.L.P. 743,
40478 DODOMA.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 26 Mei, 2018 saa 9:30 alasiri.

Imetolewa na:
Nsachris Mwamwaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
11/5/2018

About Author

Leave A Reply

Send this to a friend