Taasisi Ya Sanaa Na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)-Nafasi za Masomo Kuanzia Mwezi Aprili 2018

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Taasisi Ya Sanaa Na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)

MAOMBI YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2018/2019 KWA MUHULA UTAKAOANZA APRILI 2018

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Zamani Chuo cha Sanaa Bagamoyo) anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo kwa kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) katika fani zifuatazo.

 1. Sanaa za Maonyesho na Ufundi (Performing and Visual Arts) – Muziki, Ngoma, Uigizaji, Sarakasi, Ufundi wa Jukwaa (Stage Technology) na Sanaa za Ufundi (Fine Art).
 2. Picha Jongevu (Film and TV Production) – Uchukuaji wa Video (Video Shooting), Kuhariri Video (Video Editing), Kuongoza Filamu (Film Directing) na Uandishi Miswada ya Filamu (Script Writing).
 3. Uzalishaji wa Muziki na Sauti (Music and Sound Production) – Kurekodi Sauti (Sound Recording), Kurekodi Muziki (Music Recording), Uzalishaji wa Muziki (Music Production) na Usimamizi wa Studio (Studio Management).

CHETI MWAKA MMOJA (One year Certificate – NTA 4)

SIFA ZA KUJIUNGA

Mwombaji anatakiwa awe na sifa ifuatayo;

 • Aliyemaliza kidato cha Nne (FORM IV) na kupata Ufaulu wa kuanzia “D” Nne (4).

STASHAHADA (Two year Diploma – NTA 6)

SIFA ZA KUJIUNGA

Mwombaji anatakiwa awe na sifa moja wapo kati ya hizi zifuatazo;

 • Awe amehitimu kidato cha Sita (FORM VI) na kupata Ufaulu wa kuanzia Principal Pass Moja (1) na Subsidiary Moja (1).
 • Awe amehitimu ngazi ya Astashahada (Cheti NTA 4) kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na
 • Awe amehitimu kozi ya Ualimu Grade A.

MAELEZO MENGINE

 • Maombi yote yatumwe moja kwa moja Chuoni kwa kujaza FOMU ya maombi ambayo inapatikana Chuoni na kwenye tovuti ya Taasisi tasuba.ac.tz.
 • Gharama ya maombi ni 10, 000/= na malipo haya yatafanyika kupitia BANK ya NMB Akaunti Na. 21001100012 na jina UTAWALA CHUO CHA SANAA. Stakabadhi ya malipo (Receipt/Bank Pay Slip) itaambatanishwa pamoja na maombi ya kujiunga na Chuo.
 • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30/03/2018.
 • Kwa mawasiliano zaidi tumia anwani zifuatazo; MTENDAJI MKUU, TaSUBa,S L.P 32, BAGAMOYO, AU Barua pepe : taasisisanaa@gmail.com AU tasuba@habari.go.tz AU kwa kupitia  namba  za  simu; 
 •  +255   (0)23   2440032,   0763408792,   0655840405,   0713297626,0715974100 au 0683993401.

 

Fomu ya Maombi

Kwa maelezo zaidi bonyeza hapo chini

 

Link 1 : Tasuba Bagamoyo
Link 2: Tasuba Bagamoyo

 

About Author

Leave A Reply

Send this to a friend