Taarifa Kwa Umma Kuhusu Maombi Ya Udahili Kwa Waombaji Wa Astashahada Na Stashahada Kwa Mwaka Wa Masomo 2018/2019

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Maombi Ya Udahili Kwa Waombaji Wa Astashahada Na Stashahada Kwa Mwaka Wa Masomo 2018/2019

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi katika Vyuo Visivyokuwa Vyuo Vikuu au Vyuo Vikuu Vishiriki vinavyotoa mafunzo kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada nchini. Jukumu mojawapo la Baraza, ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo  vya Elimu ya Ufundi yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kufahamisha umma kuwa,Udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote isipokuwa za Ualimu umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 8 Juni, 2018 na utaendelea hadi tarehe 8 Septemba, 2018 kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo katika ngazi hizo.Maelekezo ya Udahili kwa kada za Ualimu yatatolewa baadaye.
Hivyo wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kutuma maombi moja kwa moja vyuoni ili kuweza kupata nafasi ya kujiunga na mafunzo kwa mwaka wa masomo wa 2018/2019. Aidha kwa wanaoomba udahili katika vyuo vya serikali vinavyotoa kozi za Afya wanaweza pia kuanya hivyo kupitia tovuti ya www.nacte.go.tz
Pia Baraza linawashauri waombaji na wazazi/walezi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye Vyuo vinavyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa mwaka wa masomo 2018/2019 (Admission Guidebook for 2018/2019 Academic year).
Mwongozo wa Udahili unapatikana katika tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz)
Kuona Mwongozo wa udahili kwa mwaka 2018/2019 (Admission Guidebook 2018/2019) bonyeza hapa
CALENDAR FOR IMPORTANT ADMISSION EVENTS FOR VARIOUS CERTIFICATE AND DIPLOMA PROGRAMMES OFFERED BY TECHNICAL INSTITUTIONS OR THE UNIVERSTIES FOR 2017/2018 AND 2018/2019 ACADEMIC YEARS

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 8/06/2018

About Author

Leave A Reply

Send this to a friend