St.Joseph University in Tanzania-Masomo ya Kompyuta ya Awali Bila Malipo

MASOMO YA KOMPYUTA YA AWALI BILA MALIPO

Katika kusaidia kuwandaa wahitimu wa shule za Sekondari ili waweze kumudu vizuri zaidi masomo
watakapojiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchini,Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Tanzania
(St. Joseph University In Tanzania)Kampasi za Mbezi-Luguruni kitaendesha bila malipo yoyote kozi ya awali
ya kompyuta (basics of computer applications) kwa muda wa wiki mbili kwa kila kundi, kuanzia tarehe 5 hadi
30 Machi, 2018. Hii ni programu mahsusi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na sita katika masomo ya
sayansi kuanzia mwaka 2015 mpaka 2018.
Usajili utafanyika tarehe 28 Februari, 2018 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi kwenye Kampasi ya Chuo Mbezi-
Luguruni.

 

Kwa mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana kupitia:
Email: admission@sjuit.ac.tz
Phone: +255 784 757010, +255 713 757010

About Author

Leave A Reply

Send this to a friend