OR-TAMISEMI:Tangazo la Nafasi za Ajira kwa Walimu wa Masomo ya Sayansi, Hisabati, Lugha (Literature in English) na Fundi Sanifu Maabara kwa Ajili ya Shule za Sekondari

Tangazo la Nafasi za Ajira kwa Walimu wa Masomo ya Sayansi, Hisabati, Lugha (Literature in English) na Fundi Sanifu Maabara kwa Ajili ya Shule za Sekondari

Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inawatangazia nafasi za kazi, Wahitimu wa fani ya Ualimu na Fundi Sanifu Maabara za Sayansi kwa ajili ya Shule za Sekondari. Waombaji wa kazi
wanapaswa kuwa ni Wahitimu wa fani hizo wa mwaka 2017 au kabla ya mwaka huo. Maombi yanapaswa kutumwa OR-TAMISEMI.
Sifa za waombaji wa nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:
1. Wahitimu wa Stashahada (Diploma) ya Ualimu mwenye kufundisha masomo ya Sayansi. Mwombaji awe na somo la kufundishia la Fizikia au Hisabati;
2. Wahitimu wa Shahada (Degree) ya Ualimu mwenye kufundisha masomo ya Sayansi. Mwombaji awe na somo la kufundishia la Fizikia au Hisabati;

3. Wahitimu wa Shahada (Degree) ya Ualimu kwa somo ya Lugha Mwombaji awe na somo la kufundishia la Literature in English; na 
4. Wahitimu wa Fundi Sanifu Maabara za Sayansi (Laboratory Technician II).
Wahitimu wote wanatakiwa kutuma maombi kwa njia ya kielektroniki kupitia kiunganishi: 196.43.65.187 (Online Teacher Employment Application System – OTEAS) katika mtandao. Nyaraka zote zitakazoambatishwa wakati
wa maombi ziwe katika mfumo wa pdf (Portable Document File). Mwombaji anatakiwa kuambatisha nyaraka zifuatazo:

(i) Barua ya maombi;
(ii) Nakala ya vyeti vya taaluma vya Kidato cha Nne na/au Kidato cha Sita;
(iii) Nakala ya Cheti cha kitaalaam (Diploma au Degree) cha kuhitimu mafunzo ya Ualimu au Fundi Sanifu Maabara ya Sayansi;
(iv) Cheti cha ulinganifu cha Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa wahitimu waliosoma nje ya Nchi; na
(v) Nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
Wahitimu wote waliowahi kutuma maombi kabla ya tangazo hili, na ambao hawajawahi kupangiwa vituo vya kazi wanashauriwa kutuma maombi upya. Kila Mhitimu anatakiwa kupendekeza Halmashauri tatu (03) za kufanyia kazi. Mwisho wa kutuma maombi hayo ni tarehe 20/07/2018.

Imetolewa na:

KATIBU MKUU
OFISI YA RAIS – TAMISEMI

About Author

Leave A Reply

Send this to a friend