Ajira Za Walimu March 2018-TAMISEMI

Ajira Za Walimu March 2018

JAMHURI YA MUUGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – TAMISEMI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUJAZA NAFASI ZA WALIMU WA AJIRA MPYA AMBAO WALIPANGIWA VITUO MWEZI DESEMBA, 2018 NA HAWAKURIPOTI

OR – TAMISEMI inapenda kuutarifu Umma kuwa, baada ya uhakiki wa uripoti wa walimu walioajiriwa Mwezi Desemba, 2017, jumla ya Walimu 45 (walimu 20 wa Shule za Msingi na 25 wa Shule za Sekondari) hawakuripoti kwenye vituo walivyopangiwa. Hivyo, OR-TAMISEMI imewapangia walimu wengine ili kujaza nafasi wazi za walimu hao katika Shule kwenye Halmashauri ambazo hawakuripoti. Walimu hao wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vya kazi ndani ya siku 14 kuanzia tarehe 17/03/2017.

Wakurugenzi wa Halmashauri wanaelekezwa kuwapokea Walimu hao na kukamilisha taratibu za ajira kwa kuzingatia taratibu na kanuni za utumishi wa Umma, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya kuripoti kwao. Taarifa ya kuripoti waajiriwa hao itumwe Ofisi ya Rais – TAMISEMI ifikapo au kabla ya tarehe 02.04.2017.

Majina ya Walimu hao waliopangiwa vituo yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI ya  www.tamisemi.go.tz

Imetolewa na:

KATIBU MKUU

A: MAPENDEKEZO YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUJAZA NAFASI ZA WALIMU AMBAO HAWAKURIPOTI KWENYE VITUO WALIVYOPANGIWA KATIKA AJIRA MPYA YA MWEZI DESEMBA, 2017

B: WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI WA AJIRA MPYA KUJAZA NAFASI ZA WALIMU AMBAO HAWAKURIPOTI KWENYE VITUO WALIVYOPANGIWA KATIKA AJIRA MPYA YA MWEZI DESEMBA, 2017

About Author

Leave A Reply

Send this to a friend