Home Announcements TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUTUMA MAOMBI YA MAFUNZO YA STASHAHADA YA...

TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUTUMA MAOMBI YA MAFUNZO YA STASHAHADA YA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2015

TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUTUMA MAOMBI YA MAFUNZO YA STASHAHADA YA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2015

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi  (NACTE) linapenda kuwataarifu wananchi kuwa limeongeza muda wa kutuma maombi ya Mafunzo ya Stashahada ya Ualimu, awamu ya pili hadi tarehe 28 Februari  2015. Baada ya tarehe hiyo, majina ya waombaji watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Stashahada ya Ualimu awamu ya pili yatatangazwa mwanzoni mwa mwezi Machi 2015 kwenye tovuti ya Baraza ambayo inaonekana katika Tangazo hili.

Watu wote wenye sifa za kujiunga na mafunzo haya wanaombwa kuitumia fursa hii muhimu kama inavyoelekezwa kwenye tovuti ya Baraza:

www.nacte.go.tz

 

Imetolewa na;

 Katibu Mtendaji

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)

Tarehe 10/2/2015