Home Announcements

NAFASI ZA MASOMO YA CHETI TAASISI YA UHASIBU TANZANIA (TIA) MWEZI FEBRUARY 2016 KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE 2015

Tangazo la nafasi za masomo kwa awamu ya pili ya mwaka wa masomo 2015/2016

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO KWA AWAMU YA PILI YA MWAKA WA MASOMO 2015/2016

MKUU WA TAASISI YA UHASIBU TANZANIA (TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) ANAWAKARIBISHA WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE MIAKA YA NYUMA NA WATAKAOMALIZA KIDATO CHA NNE MWAKA 2015, KUJIUNGA NA KOZI YA CHETI CHA AWALI YAANI BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE (NTA LEVEL 4) KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016 AWAMU YA PILI KATIKA KAMPASI ZAKE ZA DAR ES SALAAM, MBEYA, SINGIDA, MTWARA, MWANZA NA KIGOMA KWENYE FANI ZIFUATAZO:-

  • UHASIBU (ACCOUNTANCY)
  • UNUNUZI NA UGAVI (PROCUREMENT & LOGISTICS MANAGEMENT)
  • USIMAMIZI WA BIASHARA (BUSINESS ADMINISTRATION)
  • UONGOZI WA RASILIMALI WATU (HUMAN RESOURSE MANAGEMENT)
  • MASOKO & UHUSIANO (MARKETING & PUBLIC RELATIONS)
  • UHASIBU WA FEDHA ZA UMMA (PUBLIC SECTOR ACCOUNTING & FINANCE)

SIFA ZA KUJIUNGA NA KOZI ZA CHETI CHA AWALI:

Mwombaji awe amefaulu angalau masomo 3 kwa kiwango cha alama “D” au zaidi kwenye mtihani wa kidato cha nne;AuAwe na cheti cha mafunzo ya ufundi daraja la pili (NVA 2) kutoka chuo cha VETA ,mwenye ufaulu wa masomo angalau mawili katika kidato cha nne.

FOMU ZA KUJIUNGA NA CHUO ZINAPATIKANA KWENYE TOVUTI YA TAASISI www.tia.ac.tz, ZIRUDISHWE KATIKA KAMPASI ZETU ZA DSM, MBEYA, SINGIDA, MTWARA, MWANZA NA KIGOMA KUANZIA SASA NA MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI WIKI MOJA BAADA YA MATOKEO YA MTIHANI YA KIDATO CHA NNE KUTANGAZWA. MASOMO YATAANZA WIKI MOJA BAADA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KUTANGAZWA.

Kwa Mawasiliano zaidi, tafadhali piga simu namba +255 025 2502276 au 0754297971,0754 772090 au tuma baruapepe tia@tia.ac.tz,tiambeya@tia.ac.tz

STAY CONNECTED